ZANZIBAR COSMIC SOLUTION COMPANY

NAFASI YA KAZI: FUNDI UMEME WA MAGARI NA MIFUMO YA GPS

Lengo la Kazi

Tunatafuta Fundi Umeme wa Magari mwenye umakini mkubwa na ujuzi wa hali ya juu katika mifumo ya ufuatiliaji wa vyombo vya usafiri (GPS Tracking Systems). Kazi kubwa itakuwa ni kufanya wiring sahihi na salama pamoja na kusakinisha mifumo ya kudhibiti vyombo.

Majukumu Makuu

  • Kusakinisha (kufunga) GPS Tracking Devices kwenye magari, pikipiki, na mitambo mbalimbali.
  • Kusuka na kurekebisha mifumo ya mawaya (wiring) ya vyombo vya usafiri kwa usalama bila kuathiri mfumo asili wa gari.
  • Kuweka na kuunganisha Relay kwa usahihi kwa ajili ya mfumo wa kuzima na kuwasha chombo kwa mbali (Engine Immobilization/Remote Cut-off).
  • Kutambua na kutatua changamoto za kiufundi zinazojitokeza kwenye wiring au kifaa cha GPS baada ya ufungaji.

Sifa Zinazohitajika

  • Ujuzi thabiti wa kusoma na kuelewa ramani za umeme wa magari (Vehicle Wiring Diagrams), ikiwemo kutofautisha mawaya ya ACC, Power, na Ground.
  • Uzoefu wa vitendo katika matumizi ya Relay (kukatia mafuta au umeme wa gari) kwa usalama.